Mziki kwangu mi ulikuaga ndoto
Na sikuitimiza kwa kulala
Napitia nyingi changamoto
Yote kuukimbia ufukara
Kipindi naungaunga kwenye soko
Yani nasongesha miamala
Nikaona tu nijiunge na jeshi
Ili mradi na mimi niwe imara
Jeshi lilinifanya nijipinde
Ili mradi tu na mimi niwe juu
Plan nije kuwa komando Jide
Ama niwe amiri jeshi mkuu
Yalipoanza mambo ya gwaride
Hapo nikanyoosha mikono juu
Kilichofanya yanishinde
Ni matatizo ya miguu
Waliponiacha macho juu
Na kuninyamazisha mdomo
Mi nina tatizo la miguu
Wao wakaniunga mkono
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kwenye
Maisha yangu nikiacha kushukuru
Maana amani ya moyo wangu
Naomba Mungu wangu aniangazie nuru
Na nikisema nilikopita njia ilikuwa mbaya
Nitakuwa nakufuru
Huenda pengine Mungu wangu
Alipanga nipite ili nije kufaulu
Eeeeh i feel bless bless
Coz God have mercy
Hata kama ulichonacho mie sina mmmh
I feel bless bless
Coz God have mercy
Mi nilishafeli mara kadhaa
Na maisha mbona yangenishinda
Kama ningekataga tamaa eeeh
Acha nisonge mbele kwa hekima
Waliosema watasimama nami
Wamevuta kiti wamekaa
Eeeh kuna muda napitia simanzi
Usiku na mchana
Jitahidi kufanya kazi
Ipo siku utasimama
Me nimetokea uswazi
Uswahilini sana
Kwetu hakuna ugomvi
Ila waru wanapambana
Kuna muda mapenzi
Yanaweza yakakutoa kwenye reli
Maana kuna wapenzi wanapenda
Kukuona unavyofeli
Na tatizo la mapenzi
Mapenzi yana nguvu kweli kweli
Kwani ws hukusikia
Kuna mua huko ulizamisha melu eeeh
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kwenye
Maisha yangu nikiacha kushukuru
Maana amani ya moyo wangu
Naomba Mungu wangu aniangazie nuru
Na nikisema nilikopita njia ilikuwa mbaya
Nitakuwa nakufuru
Huenda pengine Mungu wangu
Alipanga nipite ili nije kufaulu
Eeeeh i feel bless bless
Coz God have mercy
Hata kama ulichonacho mie sina mmmh
I feel bless bless
Coz God have mercy