[Lyrics] Diamond Platnumz – Mbagala Lyrics

Lyrics
Mmh
Busara na upole
Na hekima niliyorithi kutoka kwa mama yangu, Mama
Vyote hukuvijali, huk’ona silingani kabisa kuwa na wewe
Kwa kuti na mkole, ukakata kabisa na shina la penzi langu mama
Eti kisa maali, ukaona bora uniache mimi na uolewe
Ile siku shekhe namuona anachoma ubani
Unavishwa pete unakua mke wa fulani
N’liumia sanaa, sanaa
Ile siku shekhe namuona anachoma ubani
Unavishwa pete unakua mke wa fulani
Niliumia sanaa, niliumia sanaa, sanaa
Tatizo kwetu mbagala, hapa nyumba mbele jalalaaa
Tatizo kwetu mbagala, uk’ona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu mbagala, hapa nyumba mbele jalalaaa
Tatizo kwetu mbagala, uk’ona mapenzi siwezi
Ungejua jinsi gani
Machozi n’livyolia kwa uchungu wa penzi langu na
Mwenzio jinsi gani, vile nimeumia moyoni
Hata kupendwa sitamani
Utamu wa mapenzi mwenzako umekula kwangu ma
Mwenzio sitamaani, hata raha tena mi sioni
Naskia hivi sasa una mtoto anaitwa mamu
Vile akinuna mpaka tabasamu
M’mefanana sana.a, sana.a
Mi mwenzako tena mapenzi mi sina hamu
Tena nna mpango wa kuhama Dar Es Salaam
Nataka niende mba.ali, niepuke vita na walimwengu
Mi mwenzenu siwezi
Tatizo kwetu mbagala, hapa nyumba mbele jalalaaa
Tatizo kwetu mbagala, uk’ona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu mbagala, hapa nyumba mbele jalalaaa
Tatizo kwetu mbagala, uk’ona mapenzi siwezi
Mbagala, mbagala, mbagala, mbagala
Uk’ona mapenzi siwezi
Mbagala (mbagala), mbagala (mbagala), mbagala (mbagala), mbagala
Uk’ona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu mbagala, hapa nyumba mbele jalalaaa
Tatizo kwetu mbagala, uk’ona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu mbagala, hapa nyumba mbele jalalaaa
Tatizo kwetu mbagala, uk’ona mapenzi siwezi
I’m back, ladies, I’m back
Bob Junior
Mr. Chocolate Flava
Yo, I’m back, Diamond, I’m back

Click to Comment

Leave a Reply

.

Designed by Admalic Inc.  BMB © 2024.

I need help with…