[Lyrics] Diamond Platnumz – Nalia Na Mengi (ft. Chidi Benz) Lyrics

Lyrics
Me niliambiwa mapenzi ni kama bahari
Ukishazama ndo basi umepotea
Kumbe mwenzangu alikuwa na tanari
Badala ya kuzama me kwangu akaelea
Akawa ananidanganya
Nikiwa nadhani ananipenda sana
Mikwanja nikamwaga mama
Japo sio kivile la kuongea manaa
Wakawa ananidanganya
Nikiwa nadhani ananipenda sana
Mbona mifedha nikamwaga mama
Japo sio kivile la kuambiwa maana
Wakaja wajinga wakamchukua
Wakamhonga honga mwisho wakamnunua
Wajinga wakamchukua
Wakamhonga honga mwisho wakamnunua (ayayayay)
Usinione nalia (rraa), usinione nalia (rraa), mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia (rraa), nalia (rraa), sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia (rraa), nalia (rraa), nalia na mengi
(Uuuh) jamani nalia (rraa), nalia (rraa), sababu ya mapenzi
Najua alimaanisha kuwa simfai ila lakini angesema
Kuliko alichofanya me akantoa nishai akanimeza akanitema
Nyie mapenzi yanauma vibaya, vibaya, vibaya
Mmmh mapenzi yanauma vibaya, vibaya, vibaya
Ile ghafla safari
Ndio inanifanya mi usingizi sipati
Huwa nakumbuka mbali
Hasa nikisikia harufu yake ya marashi
Me kwa uchungu nilivyoumia
Nikaandika hili songi la mwanduku nalia
Na vocal nikaingiza kwa hisia
Naimani iko siku nyimbo itamfikia
Me kwa uchungu nilivyoumia mie
Nikaandika songi la mwanduku nalia
Na vocal nikaingiza kwa hisia
Naimani ipo siku nyimbo itamfikia (ayayaya)
Usinione nalia (rraa), usinione nalia (rraa), mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia (rraa), nalia (rraa), sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia (rraa), nalia (rraa), nalia na mengi
(Uuuh) jamani nalia (rraa), nalia (rraa), sababu ya mapenzi
Usione nakosa raha mama nalalama kwako mara kadhaa
We ni msaada kwenye tuta so ukichomoka balaa
Sijiwezi kwangu giza naweza kimbiza na hii taa
Na hilo unajua inavyoumiza ushashuhudia mara kadhaa
We ndo urithi wakung’ang’anie ninung’unike nilie
Njia yetu moja niache nipite suka usinibanie
Kwa mahaba ya kinyamwezi na swaga zako juu
Na miguu napata picha kitandani kungfu
Uko juu ukipita lazima wasome namba
We ndo kibri fimbo kiboko ya midomo mamba
Huu ndo mfano hata unajua neno pamba sifa yake
Kwa kitambo ntakulinda kama mkinga mwenye shamba
Mikogo kila leo ntajigamba nusu soldier nusu mpweke
Kisela piga teke inauma
Usiombe mapenzi yakupige teke inauma
Usiombe mapenzi yakupige teke eeeh bounce
Usinione nalia (rraa), usinione nalia (rraa), mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia (rraa), nalia (rraa), sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia (rraa), nalia (rraa), nalia na mengi
(Uuh) jamani nalia (rraa), nalia (rraa), sababu ya mapenzi
Aaahaaaaa aaaaaahaaa aaahaaaaa
Uuuuuubuuhhuuuu aaaaaaaa aaaaaaaa aaaaa
Kikijiiiii liikikikkiiiii

Click to Comment

Leave a Reply

.

Designed by Admalic Inc.  BMB © 2024.

I need help with…