[Lyrics] Zuchu – Utaniua Lyrics

Lyrics
Eti lah lah lah lalalala lala lala
Lah lah lah lalalala lala lala
Nna hamu mwenzenu nna hamu kuyahadithia
Oh nna hamu tena nna hamu kuyasimulia
Utanii kama utani, Tulianza kimasiara
Sikudhani sikudhani, Yatafikia mahala
Akiwa hapatikani hapaliki, Sijalala
Kanifanya kitu gani, Mbona imekua mara
Dua La kuku menipata mwewe Wallahi nyinyi ni mtihani
Hata makosa ayafanye yeye mimi ndo naomba samahani
Ona anacheka kama mazuri
Anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli
Eti kumwacha naanzaje asa kusepa natoa wapi jeuri
Na kwenye koma kaeka nukta kanitia na kufulii
Oh baby mimiapa taabani (Wewee utaniua niua)
Nimeoza dah Yarrabi sihemi (Wewee utaniua niua)
Ah hizo raha zakoo (Wewee utaniua niua)
Roho yangu mali yako (Wewee utaniua niua)
Tukikosa stuli ni sunna kula kwenye mkeka
Unijue vizuri nkinuna mie ndo nadeka
Usije dhani kiburi uniache nkaja kuchekwa
Baby raha ya shughuli mkunwa awe na hekaheka
Ooh usichokipenda wewe (Aaaaah ahh)
Chunga na mimi usinifanyie (Aah aah)
Mgomba wangu mwenyewe (Ahhh ahh)
Eti ndizi nigombanie (Ahhh)
Nipe penzi nilewe niyumbe nizimie ooh ringa
Kwangu upo mwenyewe kiboko yangu mie ooh vimba
Ona Anacheka kama mazuri
Si anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli
Eti kumwacha naanzaje asa kusepa natoa wapi jeuri
Na kwenye koma kaeka nukta kanitia na kufulii
Aah eeh! baby mwenzako mimi taabani (Wewee utaniua niua)
Chagua mwenyewe unizike unisafirishee (Wewee utaniua niua)
Aah! hizo raha zakoo (Wewee utaniua niua)
Roho yangu mali yako (Wewee utaniua niua)

Click to Comment

Leave a Reply

.

Designed by Admalic Inc.  BMB © 2024.

I need help with…