[Lyrics] Ibraah – Nimpende Lyrics

Lyrics
Mmmh mmh aah ah
(Wambaga Made it)
Eh kutwa namwomba Mungu anijalie
Maumivu mbali yanipitie
Maana hayaeleweki haya, hayasomeki mapenzi
Nami nimpate wa kwangu atulie
Mwenyewe tu nijisevie
Maana hayaeleweki haya, yamejaa u-fake mapenzi
Na yasiwe ya kupostiana, na vikopakopa kwa mitandao
Tena n’choresha, tena nogesha
Chonde asiwe ya kufokafoka, mwisho yakaniacha na stress kibao
Adeke na kun’chekesha, mvua ikinyesha yeh, eeh
Asije ninyanyapaa, awe mkweli tu asijeongopa
Mwenzenu kuteswa naogopa aah
Asiwe na mipasho kama Khadija Koppa
Tupendane, wasimteke Vibopa
Yasiwe ya Konde na Wolper ah, kila siku michambo
Nataka nimpende, anipende nami nimpende
Anipende yaani nimpende eeh
Nataka nimpende eh, mwenzenu nataka nimpende
Anipende, nami nimpende, anipende yaani nimpende, anipende eeh
Anionyeshe upendo mpaka nijisahau
Yeah eh, mmh lololoh mmh
Mi nakuna kuna, mi nakuna kuna ooh
Mmmh mmh
Na asiwe wa kususasusa hata nikimwambia twende tukaoge
Asiseme nikaoge mwenyewe, mwenyewe
Na yangu asijeipangusa akili yangu, mwisho aikoroge
Awe Harmo nitakacho nipewe, nipewe mmh
Awe yangu medali aah aah
Kwa kila hali na mali
Yaani ntakesha kwa Mungu nitasali
Aah mabaya yasikupate, amwepushe
Na kitandani asiwe bonge, atamaliza godoro
Atulie, asimalize chochoro
Nisimfume, usiku wa kiza totoro
Yeh eeh tena asije ninyanyapaa
Awe mkweli tu asijeongopa
Mwenzenu kuteswa naogopa aah
Asiwe na mipasho kama Khadija Kopa
Tupendane ka Rika na Choppa
Yasiwe ya Konde na Wolper ah, kila siku michambo
Nataka nimpende, anipende nami nimpende
Anipende yaani nimpende eeh
Nataka nimupende eh, mwenzenu nataka nimpende
Anipende, nami nimpende, anipende yaani nimpende, anipende eeh
Anionyeshe upendo mpaka nijisahau
Chinga, Konde Music Worldwide
Mmh eh mmh eh (The Mix, The Mix)
Chinga, Konde Music Worldwide
Mmmh mmh

Click to Comment

Leave a Reply

.

Designed by Admalic Inc.  BMB © 2024.

I need help with…