[Lyrics] Zuchu – Mauzauza Ft. Khadija Kopa Lyrics

Lyrics
Shunuaa usijipe mapana
Eti mwili kujitutumusha
Nitakutawanya ka bahari na fimbo ya Musa
Umejigeuza Sudi sio wa Corora wala Vogi
Na hilo wowowo la kufoji eti linakupa kodii
Ohh leo unikome mwenye kiranga
(Mwenye kiranga) hujanijua vizuri
Hili timbwili la vanga (Mwenye kiranga)
Ooh leo mbona umeyabananga (Mwenye kiranga)
Mi maskini jeuri sitegemei madanga
(Mwenye kiranga) mauzauza we mwana mauzauza
Si wamekushindwa kwenu
Walimwengu tutakufunza
Mauzauza we mwana mauzauza
Si wamekushidwa kwenu walimwengu tutakufunza
Mwali kigego mwenye nyota ya mitaala
Hivi kungwi wako nani wewe? (Atajijuaaa)
Uso mitego imedoda biashara
Hueleweki si kunguru si mwewe
Wadala ubaki dala mwenzio mimi kibunda
Haufai kwa kafara si mbuzi wewe ni punda
Umejivisha ubazazi kwa mapana na marefu
Uso na kazi si wa ndala wala peku
Ooh ooh ondo ondo mlezi wa wana
We budege zoa zoa mwali pengo binti mwanya
Chuchunge kwa kudonyoa
Ooh leo unikome mwenye kiranga
(Mwenye kiranga)
Hujanijua vizuri hili timbwili la vanga
(Mwenye kiranga) ohh leo mbona umeyabananga
(Mwenye kiranga)
Me maskini jeuri, sitegemei madanga
(Mwenye kiranga) mauzauza we mwana mauzauza
Si wamekushindwa kwenu
Walimwengu tutakufunza
Mauzauza we mwana mauzauza
Si wamekushidwa kwenu walimwengu tutakufunza
Hutayaweza yangu yako yanakushinda
Hutayaweza yangu yako yanakushinda
Hutayaweza yangu yako yanakushinda
Hutayaweza yangu yako yanakushinda
Hutayaweza yangu yako yanakushinda
Hutayaweza yangu yako yanakushinda

Click to Comment

Leave a Reply

.

Designed by Admalic Inc.  BMB © 2024.

I need help with…