[Lyrics] Diamond Platnumz – Nawaza Lyrics

Lyrics
Nawa nawa
Nawa nawaza tu
Nawa nawa
Nawa nawaza tu
Nawaza pru mpaka maka Ruge amerudi tena
Je kwa huu mziki wa
Sasa sijui nini angesema!?
Na nimejifunza binadamu kweli hawana jema
Yani mtoto unaemtunza ndo anakuombea ukilema
Nashangaa
Nawaza Vanny na Elizabeth, clip zao zikivuja
Ndoa itaimarika eti, au ndo ataifoja?!
Nawaza muchana, usiku jibu halifiki
Wanaonitukana, tuna bifu au ilimradi kiki?!
Nawaza kina Kimambi bwana
Wangekua wagawa ridhiki
Hivi kweli ningejulikana si
Wangenizima nsisike
Nlowaza leo nshawaza sana kina
Kiba ugomvi kipi?!
Nikagundua ni ushamba na ujana
Wa kugombania mashabiki
Nawa nawa
Nawa nawaza tu
Nawa nawa
Nawa nawaza tu
Oh nawaza
Huenda Steven Kanumba angelikuwepo hai
Nawaza movie zetu pia tungejidai
Nawaazaa hivi kombe la dunia hatufikagi why?!
Nawaza, tatizo ni team au uongozi haufai
Mawazo mengine mtanange bora
Tuache yataleta ukakasi
Je angekuepo Muzee Nyange
Uncle Shamte angepata nafasi?!
Nawaza ka ngеkua na Wema Sepetu hadi lеo
Sijui ngekua nshafulia au zaidi maendeleo
Oh nawaza siku nikifa sijui wasafi itakufa
Nawaza sijui maradhi ama ajali itanikuta
Nawaza oh Mama Dangote nani chozi atamfuta
Nawaza sijui nyimbo zangu watazikumbuka, eeh
Nlowaza leo nshawaza sana
Nnachoshindwa kuwa kipi
Nikagundua naepusha lawama maana
Najijua kwa kucheat
Nawa nawa
Nawa nawaza tu
Nawa nawa
Nawa nawaza tu

Click to Comment

Leave a Reply

.

Designed by Admalic Inc.  BMB © 2024.

I need help with…