[Lyrics] Harmonize – Utanikumbuka Lyrics

Lyrics
Big Boy On The Beat
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Natamani kuimba
Pengine ukasikia
Maneno yangu ya mwisho
Ila sauti ndo inagoma
Yani kama inakwaruza
Huruma
Ukinitazama machoni yamevimba
Nimekesha nalia
Na sijui lini mwisho
Mwili wa joto na homa
Yani mpaka naunguza
Mapenzi hayana dhihaki
Mwenzako nishawaza hadi faraki
Ama niende kortini nikashitaki
Kwamba unadhulumu furaha yangu
Mdomoni una maji we samaki
Sa mbona hata kusema hutaki
Ama ndo unataka sitaki
Ina maana huzioni jitihada zangu
Pengine donda nililokupa
Limefuta upendo
Unajaribu kujilazimisha
Mengine unafanya kuniridhisha
Mwili umekonda umebaki mifupa
Kulilia upendo
Basi moyo rudisha
Kama umenisamehe na yameisha
Kinyonge ninajiuliza bila majibu
Wapi nitapoharibu
Kila ninachojaribu hakikupendezi
Utanikumbuka mpenzi uta…
Utanikumbuka mpenzi uta…
(Utanikumbuka mpenzi uta…)
Maana wapo watakaokukosea
Na wasikiri kosa
Muda wote wanawaza kukuchezea
Hakuna wa kukuposa
Eeh eeh
Inaboa mapenzi yakishaisha
Licha ya kujitoa
Mwenzangu kumridhisha
Eti mara yupo bize yupo bize
Alipo hataki nimuulize
Anajua lazima iniumize
Imeandikwa samehe na usilipize
Huenda hata msamaha ulionipa ni kazi bure
Kama umeshindwa nifanya
Nijione kama yule
Rajabu wa zamani
Rudi Ma unipe joto
Hili baridi kama Toronto
Si ulijiita Kurwa mi Doto
Na utanipa watoto
Sa mbona sikuoni
Ninajiuliza bila majibu
Wapi nitapoharibu
Kila ninachojaribu
Hakikupendezi
Utanikumbuka mpenzi uta…
Utanikumbuka mpenzi uta…
(Utanikumbuka mpenzi uta…)
Maana wapo watakaokukosea
Na wasikiri kosa
Muda wote wanawaza kukuchezea
Hakuna wa kukuposa
Eeh eeh
Konde Boy Call Me Number mber One, Bakhresa
Uuh Uuh Uuh Utanikumbuka…
Uuh Uuh Uuh Utanikumbuka…
Na sikuombei mabaya
(Uuh Uuh Uuh Utanikumbuka…)
Ooh Mabaya
Na sitakusema vibaya
(Uuh Uuh Uuh Utanikumbuka…)
Uso umeumbwa na haya
Uncle Duke unipigie ukinikumbuka

Click to Comment

Leave a Reply

.

Designed by Admalic Inc.  BMB © 2024.

I need help with…